Hosea 11
Upendo Wa Mungu Kwa Israeli
1 a“Wakati Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda,nilimwita mwanangu kutoka Misri.
2 bLakini kadiri nilivyomwita Israeli,
ndivyo walivyokwenda mbali nami.
Walitoa dhabihu kwa Mabaali
na kufukiza uvumba kwa vinyago.
3 cMimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea,
nikiwashika mikono;
lakini hawakutambua
kuwa ni mimi niliyewaponya.
4 dNiliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu,
kwa vifungo vya upendo;
niliondoa nira shingoni mwao
nami nikainama kuwalisha.
5 e“Je, hawatarudi Misri,
nayo Ashuru haitawatawala
kwa sababu wamekataa kutubu?
6 fPanga zitametameta katika miji yao,
zitaharibu makomeo ya malango yao
na kukomesha mipango yao.
7 gWatu wangu wamedhamiria kuniacha.
Hata kama wakimwita Yeye Aliye Juu Sana,
kwa vyovyote hatawainua.
8 h“Efraimu, ninawezaje kukuacha?
Ee Israeli, ninawezaje kukutoa?
Nitawezaje kukutendea kama Adma?
Nitawezaje kukufanya kama Seboimu?
Moyo wangu umegeuka ndani yangu,
huruma zangu zote zimeamshwa.
9 iSitatimiza hasira yangu kali,
wala sitageuka na kumharibu Efraimu.
Kwa kuwa mimi ndimi Mungu,
wala si mwanadamu,
Aliye Mtakatifu miongoni mwenu.
Sitakuja kwa ghadhabu.
10 jWatamfuata Bwana;
atanguruma kama simba.
Wakati angurumapo,
watoto wake watakuja wakitetemeka
kutoka magharibi.
11 kWatakuja wakitetemeka
kama ndege wakitoka Misri,
kama hua wakitoka Ashuru.
Nitawakalisha katika nyumba zao,”
asema Bwana.
Dhambi Ya Israeli
12 lEfraimu amenizunguka kwa uongo,nyumba ya Israeli kwa udanganyifu.
Naye Yuda ni mkaidi dhidi ya Mungu,
hata kinyume cha yule mwaminifu Aliye Mtakatifu.
Copyright information for
SwhNEN