Job 27
Hotuba Ya Mwisho Ya Ayubu
Ayubu Anadumisha Uadilifu Wake
1 aNdipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:2 b“Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu,
Mwenyezi ambaye amenifanya
nionje uchungu wa nafsi,
3 ckwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu,
nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu,
4 dmidomo yangu haitanena uovu,
wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
5 eSitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi;
hadi nife, sitakana uadilifu wangu.
6 fNitadumisha haki yangu wala sitaiacha;
dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.
7“Watesi wangu wawe kama waovu,
nao adui zangu wawe kama wasio haki!
8 gKwa maana mtu asiyemcha Mungu
analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali,
Mungu anapouondoa uhai wake?
9 hJe, Mungu husikiliza kilio chake,
shida zimjiapo?
10 iJe, anaweza kumfurahia Mwenyezi?
Je, atamwita Mungu nyakati zote?
11 j“Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu;
njia za Mwenyezi sitazificha.
12Ninyi nyote mmeona hili wenyewe.
Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?
13 k“Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu,
urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi:
14 lHata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani,
fungu lao ni kuuawa kwa upanga;
wazao wake hawatakuwa kamwe
na chakula cha kuwatosha.
15 mTauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao,
nao wajane wao hawatawaombolezea.
16 nAjapokusanya fedha nyingi kama mavumbi,
na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,
17 oyale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa,
naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.
18 pNyumba aijengayo ni kama utando wa buibui,
kama kibanda alichotengeneza mlinzi.
19 qYeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho;
afunguapo macho yake, yote yametoweka.
20 rVitisho humjia kama mafuriko;
dhoruba humkumba ghafula usiku.
21 sUpepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka;
humzoa kutoka mahali pake.
22 tHumvurumisha bila huruma,
huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.
23 uUpepo humpigia makofi kwa dharau,
na kumfukuza atoke mahali pake.
Copyright information for
SwhNEN