‏ Proverbs 16

1 aMipango ya moyoni ni ya mwanadamu,
bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.

2 bNjia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe,
bali makusudi hupimwa na Bwana.

3 cMkabidhi Bwana lolote ufanyalo,
nayo mipango yako itafanikiwa.

4 d Bwana hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe;
hata waovu kwa siku ya maangamizi.

5 e Bwana huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo.
Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.

6 fKwa upendo na uaminifu uovu huondolewa;
kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya.

7 gNjia za mtu zinapompendeza Bwana,
huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani.

8 hAfadhali kitu kidogo pamoja na haki
kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.

9 iMoyo wa mtu huifikiri njia yake,
bali Bwana huelekeza hatua zake.

10 jMidomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu,
wala kinywa chake hakipotoshi haki.

11 kVipimo na mizani za halali hutoka kwa Bwana;
mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye.

12 lWafalme huchukia sana kutenda maovu,
kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kwa njia ya haki.

13 mWafalme hufurahia midomo ya uaminifu;
humthamini mtu asemaye kweli.

14 nGhadhabu ya mfalme ni mjumbe wa mauti,
bali mtu mwenye hekima ataituliza.

15 o pUso wa mfalme ungʼaapo, inamaanisha uhai;
upendeleo wake ni kama wingu la mvua wakati wa vuli.

16 qNi bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu,
kuchagua ufahamu kuliko fedha!

17 rNjia kuu ya wanyofu huepuka ubaya;
yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake.

18 sKiburi hutangulia maangamizi,
roho ya majivuno hutangulia maanguko.

19Ni afadhali kuwa mnyenyekevu katika roho
miongoni mwa walioonewa
kuliko kugawana nyara pamoja na wenye kiburi.

20 tYeyote anayekubali mafundisho hustawi,
tena amebarikiwa yeye anayemtumaini Bwana.

21 uWenye hekima moyoni huitwa wenye ufahamu,
na maneno ya kupendeza huchochea mafundisho.

22 vUfahamu ni chemchemi ya uzima kwa wale walio nao,
bali upumbavu huleta adhabu kwa wapumbavu.

23 wMoyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake,
na midomo yake huchochea mafundisho.

24 xManeno ya kupendeza ni kama sega la asali,
ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.

25 yIko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,
bali mwisho wake huelekeza mautini.

26 zShauku ya mfanyakazi humhimiza kufanya kazi;
njaa yake humsukuma aendelee.

27 aaMtu mbaya kabisa hupanga mabaya,
maneno yake ni kama moto uunguzao.

28 abMtu mpotovu huchochea ugomvi,
nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.

29Mtu mkali humvuta jirani yake
na kumwongoza katika mapito yale mabaya.

30 acYeye akonyezaye kwa jicho lake anapanga upotovu;
naye akazaye midomo yake amenuia mabaya.

31 adMvi ni taji ya utukufu;
hupatikana kwa maisha ya uadilifu.

32 aeNi afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa,
mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji.

33 afKura hupigwa kwa siri,
lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.
Copyright information for SwhNEN