‏ Proverbs 22

1 aHeri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi,
kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu.

2 bTajiri na maskini wanafanana kwa hili:
Bwana ni Muumba wao wote.

3 cMtu mwenye busara huona hatari na kujificha,
bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa.

4 dUnyenyekevu na kumcha Bwana
huleta utajiri, heshima na uzima.

5 eKatika mapito ya waovu kuna miiba na mitego,
bali yeye ailindaye nafsi yake hukaa mbali nayo.

6 fMfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,
naye hataiacha hata akiwa mzee.

7 gMatajiri huwatawala maskini
naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye.

8 hYeye aupandaye uovu huvuna taabu,
nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa.

9 iMtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa
kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini.

10 jMfukuze mwenye dhihaka,
na mvutano utatoweka;
ugomvi na matukano vitakoma.

11 kYeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema,
mfalme atakuwa rafiki yake.

12Macho ya Bwana hulinda maarifa,
bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu.

13 lMvivu husema, “Yuko simba nje!”
au, “Nitauawa katika mitaa!”

14 mKinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu;
yeye aliye chini ya ghadhabu ya Bwana
atatumbukia ndani yake.

15 nUpumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,
bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.

16 oYeye amwoneaye maskini ili kujiongezea mali,
naye ampaye tajiri zawadi, wote huwa maskini.

Misemo Ya Wenye Hekima

17 pTega sikio na usikie misemo ya wenye hekima,
elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo,
18kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako
na kuwa nayo yote tayari midomoni mwako.
19Ili tumaini lako liwe katika Bwana,
hata wewe, ninakufundisha leo.
20 qJe, sijakuandikia misemo thelathini,
misemo ya mashauri na maarifa,
21 rkukufundisha maneno ya kweli na ya kuaminika,
ili uweze kutoa majibu sahihi
kwake yeye aliyekutuma?

22 sUsiwadhulumu maskini kwa sababu ni maskini,
wala kumdhulumu mhitaji mahakamani,
23 tkwa sababu Bwana atalichukua shauri lao
naye atawateka wao waliowateka.

24Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka,
usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika,
25 ula sivyo utajifunza njia zake
na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego.

26 vUsiwe mwenye kupana mikono katika rehani,
au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni.
27 wKama ukikosa njia ya kulipa,
kitanda chako
kitachukuliwa ukiwa umekilalia.

28 xUsisogeze jiwe la mpaka wa zamani
lililowekwa na baba zako.

29 yJe, unamwona mtu stadi katika kazi yake?
Atahudumu mbele ya wafalme;
hatahudumu mbele ya watu duni.
Copyright information for SwhNEN