‏ Psalms 10

Sala Kwa Ajili Ya Haki

1 aKwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali?
Kwa nini unajificha wakati wa shida?

2 bKatika kiburi chake, mwovu humtesa maskini,
waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.
3Hujivunia tamaa za moyo wake;
humbariki mlafi na kumtukana Bwana.
4 cKatika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu,
katika mawazo yake yote
hakuna nafasi ya Mungu.
5 dNjia zake daima hufanikiwa;
hujivuna na amri zako ziko mbali naye,
huwacheka kwa dharau adui zake wote.
6 eAnajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa,
daima nitakuwa na furaha,
kamwe sitakuwa na shida.”
7 fKinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho;
shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.
8 gHuvizia karibu na vijiji;
kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia,
akivizia wapitaji.
9 hHuvizia kama simba aliye mawindoni;
huvizia kumkamata mnyonge,
huwakamata wanyonge na kuwaburuza
katika wavu wake.
10 iMateka wake hupondwa, huzimia;
wanaanguka katika nguvu zake.
11 jAnajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau,
huficha uso wake na haoni kabisa.”

12 kInuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu.
Usiwasahau wanyonge.
13 lKwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu?
Kwa nini anajiambia mwenyewe,
“Hataniita nitoe hesabu?”
14 mLakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni,
umekubali kuyapokea mkononi mwako.
Mhanga anajisalimisha kwako,
wewe ni msaada wa yatima.
15 nVunja mkono wa mtu mwovu na mbaya,
mwite atoe hesabu ya maovu yake
ambayo yasingejulikana.

16 o Bwana ni Mfalme milele na milele,
mataifa wataangamia watoke nchini mwake.
17 pUnasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa,
wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,
18 qukiwatetea yatima na walioonewa,
ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena.
Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.