Psalms 105
Uaminifu Wa Mungu Kwa Israeli
(1 Nyakati 16:8-22)
1 aMshukuruni Bwana, liitieni jina lake,wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.
2 bMwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa,
waambieni matendo yake yote ya ajabu.
3 cLishangilieni jina lake takatifu,
mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.
4 dMtafuteni Bwana na nguvu zake,
utafuteni uso wake siku zote.
5 eKumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,
miujiza yake na hukumu alizozitamka,
6 fenyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake,
enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
7 gYeye ndiye Bwana Mungu wetu,
hukumu zake zimo duniani pote.
8 hHulikumbuka agano lake milele,
neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
9 iagano alilolifanya na Abrahamu,
kiapo alichomwapia Isaki.
10 jAlilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,
kwa Israeli liwe agano la milele:
11 k“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani
kuwa sehemu utakayoirithi.”
12 lWalipokuwa wachache kwa idadi,
wachache sana na wageni ndani yake,
13 mwalitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,
kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
14 nHakuruhusu mtu yeyote awaonee;
kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
15 o“Msiwaguse niliowatia mafuta;
msiwadhuru manabii wangu.”
16 pAkaiita njaa juu ya nchi
na kuharibu chakula chao chote,
17 qnaye akatuma mtu mbele yao,
Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa.
18 rWalichubua miguu yake kwa minyororo,
shingo yake ilifungwa kwa chuma,
19 shadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia,
hadi neno la Bwana lilipomthibitisha.
20 tMfalme alituma watu wakamfungua,
mtawala wa watu alimwachia huru.
21Alimfanya mkuu wa nyumba yake,
mtawala juu ya vyote alivyokuwa navyo,
22 ukuwaelekeza wakuu wa mfalme apendavyo
na kuwafundisha wazee wake hekima.
23 vKisha Israeli akaingia Misri,
Yakobo akaishi kama mgeni katika nchi ya Hamu.
24 w Bwana aliwafanya watu wake kuzaana sana,
akawafanya kuwa wengi sana kuliko adui zao,
25 xndiye aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake,
wakatenda hila dhidi ya watumishi wake.
26 yAkamtuma Mose mtumishi wake,
pamoja na Aroni, aliyemchagua.
27 zWalifanya ishara zake za ajabu miongoni mwao,
miujiza yake katika nchi ya Hamu.
28 aaAlituma giza na nchi ikajaa giza,
kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake?
29 abAligeuza maji yao kuwa damu,
ikasababisha samaki wao kufa.
30 acNchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia
hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao.
31 adAlisema, yakaja makundi ya mainzi,
na viroboto katika nchi yao yote.
32 aeAlibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe,
yenye umeme wa radi nchini yao yote,
33 afakaharibu mizabibu yao na miti ya tini,
na akaangamiza miti ya nchi yao.
34 agAlisema, nzige wakaja,
tunutu wasio na idadi,
35wakala kila jani katika nchi yao,
wakala mazao ya ardhi yao.
36 ahKisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao,
matunda ya kwanza ya ujana wao wote.
37 aiAkawatoa Israeli katika nchi
wakiwa na fedha na dhahabu nyingi,
wala hakuna hata mmoja
kutoka kabila zao aliyejikwaa.
38 ajMisri ilifurahi walipoondoka,
kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia.
39 akAlitandaza wingu kama kifuniko,
na moto kuwamulikia usiku.
40 alWaliomba, naye akawaletea kware,
akawashibisha kwa mkate wa mbinguni.
41 amAlipasua mwamba, maji yakabubujika,
yakatiririka jangwani kama mto.
42 anKwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu,
aliyompa Abrahamu mtumishi wake.
43 aoAliwatoa watu wake kwa furaha,
wateule wake kwa kelele za shangwe,
44 apakawapa nchi za mataifa, wakawa warithi
wa mali wengine walikuwa wameitaabikia:
45 aqalifanya haya ili wayashike mausia yake
na kuzitii sheria zake.
Msifuni Bwana. ▼
▼Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.
Copyright information for
SwhNEN