c Za 4:1; 26:11; 61:2; 77:3; 142:3; Yer 3:12; 8:18; 12:15; 31:20; Hos 6:1; Isa 40:31; Za 32:3; 38:3; 42:10; 102:3
d Ay 7:11; Za 4:2; 31:7; 38:8; 55:4; 89:46; Yn 12:27; Isa 6:11; Rum 9:2; 2Kor 2:4; Hab 1:12; 1Sam 1:14; 1Fal 18:21; Yer 4:14; Mt 26:38; Mit 18:14
Psalms 6
Sala Kwa Ajili Ya Msaada Wakati Wa Taabu
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi. ▼▼Sheminithi ni mtajo mmojawapo katika lugha ya uimbaji. Zaburi ya Daudi.
1 bEe Bwana, usinikemee katika hasira yako,wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.
2 cUnirehemu Bwana,
kwa maana nimedhoofika;
Ee Bwana, uniponye,
kwa maana mifupa yangu
ina maumivu makali.
3 dNafsi yangu ina uchungu mwingi.
Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini?
4 eGeuka Ee Bwana, unikomboe,
uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.
5 fHakuna mtu anayekukumbuka
akiwa amekufa.
Ni nani awezaye kukusifu
akiwa kuzimu?
6 gNimechakaa kwa kulia kwa huzuni;
usiku kucha nafurikisha
kitanda changu kwa machozi;
nimelowesha viti vyangu vya fahari
kwa machozi.
7 hMacho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,
yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.
8 iKaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,
kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu.
9 j Bwana amesikia kilio changu kwa huruma,
Bwana amekubali sala yangu.
10 kAdui zangu wote wataaibika na kufadhaika,
watarudi nyuma kwa aibu ya ghafula.
Copyright information for
SwhNEN