2 Kings 20:1-3
Ugonjwa Wa Hezekia
(2 Nyakati 32:24-26; Isaya 38:1-8, 21-22)
1Katika siku hizo, Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo Bwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”2Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana: 3 a“Ee Bwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu.
Copyright information for
SwhNEN