‏ Deuteronomy 27:15-26

15 a“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
16 b“Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
17 c“Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
18 d“Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
19 e“Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
20 f“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
21 g“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama yeyote.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
22 h“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
23 i“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe wake.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
24 j“Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
25 k“Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumuua mtu asiye na hatia.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
26 l“Alaaniwe mtu yule ambaye hatashikilia maneno ya sheria hii kwa kuyatekeleza.”


Kisha watu wote watasema, “Amen!”
Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.