aKum 32:16; Amu 2:14; 20; 10:7; 2Fal 13:3; 22:13; Za 106:29, 40; Yer 7:18; 21:5; 36:17; Amu 6:13; 2Nya 15:2; 24:20; Ezr 8:22; Za 44:9; Isa 2:6; Kum 32:20; Isa 1:15; 45:15; 53:3; 54:8; Ay 13:24; Za 13:1; 27:9; 30:7; 104:29; Isa 50:6; Yer 33:5; Eze 39:29; Mik 3:4; Yer 4:20; Eze 7:26; Hes 14:42; Hos 9:12
Deuteronomy 31:17-21
17 aSiku hiyo nitawakasirikia na kuwaacha; nitawaficha uso wangu, nao wataangamizwa. Maafa mengi na shida nyingi zitakuja juu yao, nao siku hiyo watauliza, ‘Je, maafa haya hayakuja juu yetu kwa sababu Mungu wetu hayuko pamoja nasi?’ 18Nami hakika nitauficha uso wangu siku hiyo kwa sababu ya maovu yao yote kwa kugeukia miungu mingine.19 b“Sasa ujiandikie wimbo huu, ▼
▼Wimbo huu hapa ina maana wimbo wa Mose.
uwafundishe Waisraeli na uwaamuru wauimbe, ili upate kuwa ushahidi wangu dhidi yao. 20 dNitakapokwisha kuwaingiza katika nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi niliyowaahidi baba zao kwa kiapo, nao watakapokula wakashiba na kufanikiwa, watageukia miungu mingine na kuiabudu, wakinikataa mimi na kuvunja Agano langu. 21 eMaafa na shida zitakapokuja juu yao, wimbo huu utashuhudia dhidi yao, kwa sababu hautasahauliwa na wazao wao. Ninajua lile wanaloandaa kufanya, hata kabla sijawaingiza katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo.”
Copyright information for
SwhNEN