e Mwa 4:24; Yer 51:6; Mwa 30:2; Kut 32:34; Za 54:5; Rum 12:19; Ebr 10:30; Za 17:5; 35:6; 37:31; 38:16; 66:9; 73:2; 94:18; 121:3; Mit 4:19; Yer 23:12; Eze 7:8-9
Deuteronomy 32:31-37
31 aKwa kuwa mwamba wao si kama Mwamba wetu,sawasawa na vile adui zetu wanavyokiri.
32 bMzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma,
na kutoka kwenye mashamba ya Gomora.
Zabibu zake zimejaa sumu,
na vishada vyake vimejaa uchungu.
33 cMvinyo wao ni sumu ya nyoka,
sumu yenye kufisha ya swila.
34 d“Je, hili sikuliweka akiba
na kulifungia kwenye vyumba vyangu vya hazina?
35 eNi juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza.
Wakati utakapowadia, mguu wao utateleza;
siku yao ya maafa ni karibu,
na maangamizo yao yanawajia haraka.”
36 f Bwana atawahukumu watu wake,
na kuwahurumia watumishi wake
atakapoona nguvu zao zimekwisha
wala hakuna yeyote aliyebaki,
mtumwa au aliye huru.
37 gAtasema: “Sasa iko wapi miungu yao,
mwamba walioukimbilia,
Copyright information for
SwhNEN