Ecclesiastes 2:11-22
11Hata hivyo nilipokuja kuangalia yote ambayomikono yangu ilikuwa imefanya
na yale niliyotaabika kukamilisha,
kila kitu kilikuwa ni ubatili, ni kukimbiza upepo;
hapakuwa na faida yoyote chini ya jua.
Hekima Na Upumbavu Ni Ubatili
12Kisha nikageuza mawazo yangu kufikiria hekima,wazimu na upumbavu.
Ni nini zaidi mtu anayetawala baada ya mfalme
anachoweza kufanya ambacho hakijafanywa?
13 aNikaona kuwa hekima ni bora kuliko upumbavu,
kama vile nuru ilivyo bora kuliko giza.
14 bMtu mwenye hekima ana macho katika kichwa chake,
lakini mpumbavu anatembea gizani;
lakini nikaja kuona kwamba
wote wawili hatima yao inafanana.
15 cKisha nikafikiri moyoni mwangu,
“Hatima ya mpumbavu itanipata mimi pia.
Nitafaidi nini basi kwa kuwa na hekima?”
Nikasema moyoni mwangu,
“Hili nalo ni ubatili.”
16 dKwa maana kwa mtu mwenye hekima,
kama ilivyo kwa mpumbavu,
hatakumbukwa kwa muda mrefu,
katika siku zijazo wote watasahaulika.
Kama vile ilivyo kwa mpumbavu,
mtu mwenye hekima pia lazima atakufa!
Kutaabika Ni Ubatili
17Kwa hiyo nikachukia maisha, kwa sababu kazi inayofanyika chini ya jua ilikuwa masikitiko kwangu. Yote hayo ni ubatili, ni kukimbiza upepo. 18 eNikachukia kila kitu nilichokuwa nimetaabikia chini ya jua, kwa sababu ni lazima nimwachie yule ajaye baada yangu. 19Nani ajuaye kama atakuwa ni mtu mwenye hekima au mpumbavu? Lakini hata hivyo yeye ndiye atakayetawala kazi zote ambazo nimemiminia juhudi na ustadi chini ya jua. Hili nalo ni ubatili. 20Kwa hiyo moyo wangu ukaanza kukata tamaa juu ya kazi yangu yote niliyoifanya kwa taabu chini ya jua. 21Kwa kuwa mtu anaweza kufanya kazi yake kwa hekima, maarifa na ustadi, kisha analazimika kuacha vyote alivyo navyo kwa mtu mwingine ambaye hajavifanyia kazi. Hili nalo pia ni ubatili tena ni balaa kubwa. 22 fMtu atapata nini kwa taabu yote na kuhangaika kwa bidii katika kazi anayotaabikia chini ya jua?
Copyright information for
SwhNEN