c Kut 32:8; 34:17; Law 19:4; 26:1; Kum 4:15-23; 27:15; 2Sam 7:22; 1Fal 14:9; 2Fal 17:12; Isa 42:8; 44:9
Exodus 20:2-7
2 a“Mimi ndimi Bwana Mungu wako, niliyekutoa Misri, kutoka nchi ya utumwa.3 bUsiwe na miungu mingine ila mimi.
4 cUsijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. 5 dUsivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 elakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.
7 fUsilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.
Copyright information for
SwhNEN