Exodus 30:1-5
Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba
(Kutoka 37:25-28)
1 a“Tengeneza madhabahu kwa mbao za mshita kwa ajili ya kufukizia uvumba. 2 bMadhabahu hayo yawe mraba, urefu na upana wake dhiraa moja, ▼▼Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.
na kimo cha dhiraa mbili, ▼▼Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90.
nazo pembe zake zitakuwa kitu kimoja nayo. 3 eFunika hayo madhabahu juu na pande zote na pia pembe zake kwa dhahabu safi, na uifanyizie ukingo wa dhahabu kuizunguka. 4 fTengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, ziwe mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko itumikayo kuibebea madhabahu. 5 gTengeneza mipiko kwa miti ya mshita na uifunike kwa dhahabu.
Copyright information for
SwhNEN