Exodus 37:1-9
Sanduku La Agano
(Kutoka 25:10-22)
1 aBezaleli akatengeneza Sanduku la mbao za mshita: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, ▼▼Dhiraa moja na nusu ni sawa na mita 1.13.
upana wake dhiraa moja na nusu, na kimo chake dhiraa moja na nusu. 2Akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulizungushia ukingo wa dhahabu. 3Akasubu pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 4 cKisha akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 5 dAkaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. 6 eAkatengeneza kifuniko cha upatanisho kwa dhahabu safi: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu. 7 fKisha akatengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. 8Akatengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; akawatengeneza kuwa kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. 9 gMakerubi hao walikuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, wakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao walielekeana, wakitazama hicho kifuniko.
Copyright information for
SwhNEN