Exodus 37:10-24
Meza
(Kutoka 25:23-30)
10 aAkatengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili, ▼▼Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90.
upana wa dhiraa moja, ▼▼Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.
na kimo cha dhiraa moja na nusu. 11Kisha akaifunika kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. 12Pia akatengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne, ▼▼Nyanda nne ni sawa na sentimita 8.
na kuufanyia ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. 13Akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na kuzifungia kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. 14 ePete hizo ziliwekwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko iliyotumika kuibebea hiyo meza. 15Mipiko hiyo ya kubebea meza ilitengenezwa kwa mti wa mshita, na ilikuwa imefunikwa kwa dhahabu. 16 fVyombo vyote vya mezani vilitengenezwa kwa dhahabu safi: yaani sahani zake, masinia, na bakuli na bilauri zake kwa ajili ya kumiminia sadaka za vinywaji. Kinara Cha Taa
(Kutoka 25:31-40)
17 gAkatengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vilivyofanana na ua, matovu na maua vilikuwa kitu kimoja. 18Matawi sita yalitokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. 19Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vilikuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yaliyotokeza kwenye kile kinara cha taa. 20 hJuu ya kinara chenyewe kulikuwepo na vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi yakiwa na matovu yake na maua yake. 21Tovu moja lilikuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani, matawi sita kwa jumla. 22 iMatovu na matawi yote yalikuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakiwa yamefuliwa kwa dhahabu safi.23 jAkatengeneza taa zake saba, na pia mikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote kwa dhahabu safi. 24Akatengeneza kinara hicho cha taa pamoja na vifaa vyake vyote kutumia talanta ▼
▼Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34.
moja ya dhahabu safi.
Copyright information for
SwhNEN