Ezekiel 32:2-3
2 a“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie:“ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa,
wewe ni kama joka kubwa baharini,
unayevuruga maji kwa miguu yako
na kuchafua vijito.
3 b“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Nikiwa pamoja na wingi mkubwa wa watu
nitautupa wavu wangu juu yako,
nao watakukokota katika wavu wangu.
Copyright information for
SwhNEN