d Eze 27:7, 10, 12, 25; 38:13; Za 48:7; 72:10; Isa 2:16; 23:1-6, 12; 66:19; Yer 2:10; 10:9; Yon 1:3; Hes 24:24; Dan 11:30
e 2Fal 19:9; Nah 3:9; 2Nya 12:3; 16:8; Isa 11:11; 18:1; 20:3; 43:3; Yer 46:9; Eze 27:10; 30:4-9; 38:5; Mwa 9:18; Sef 2:12; 3:10
g Isa 21:13; 43:3; 60:6; Mwa 2:11; 25:3; Eze 38:13; 27:15, 20, 22; 1Fal 10:1; 2Nya 9:1; Ay 1:15; 6:19; 16:11; Za 72:10; Yer 25:23-24; 6:20; 49:8; Yoe 3:8; 1Nya 1:32
m Mwa 9:18; 5:20; 23:3; 25:10; 26:34; 27:46; 49:32; Yos 1:4; 11:8; Amu 10:6; Isa 23:2-4; Yer 25:22; 27:3; 47:4; Eze 16:3; 28:21; 32:30; Yoe 3:4; Zek 9:2; Kut 4:22; Hes 1:20; 3:2; 13:29; 18:15; 33:4; 1Sam 26:6
nAmu 19:10; 1Nya 11:4; Ezr 9:1; Kut 3:8; 2Nya 8:7; Hes 13:29; 21:13; 32:39; Yos 2:10; Kum 1:4; 7:1; Yos 2:10; Mwa 15:18-21
pEze 27:8; 1Nya 18:3; Mwa 12:6; 13:17; 50:11; Kut 13:11; Hes 13:29; 14:25; 21:3; 33:40; Kum 7:1; Amu 1:1
qMwa 11:31; 12:1; 13:12; 14:2; 17:8; 24:3; 26:34; 37:1; 27:46; 28:1-8; 31:18; 35:6; 49:13; Law 25:38; Yos 19:28; Amu 1:18, 31; 18:28; 6:4; 16:1, 21; 2Nya 24:6; 14:13; Kum 2:23; 29:23; Yos 10:41; 11:22; 15:47; 1Sam 6:17; Yer 25:20; 47:1; Amo 1:6; Sef 2:4
Genesis 10
Mataifa Yaliyotokana Na Noa
(1 Nyakati 1:5-23)
1 aHawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.Wazao Wa Yafethi
2 bWana wa Yafethi walikuwa:Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
3 cWana wa Gomeri walikuwa:
Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
4 dWana wa Yavani walikuwa:
Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. 5(Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)
Wazao Wa Hamu
6 eWana wa Hamu walikuwa:Kushi, Misraimu, ▼
▼Yaani Misri.
Putu na Kanaani.7 gWana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.
8 hKushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani. 9 iAlikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.” 10 jVituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari. 11 kKutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala, 12na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.
13Misraimu alikuwa baba wa:
Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 14 lWapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.
15 mKanaani alikuwa baba wa:
Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, 16 nWayebusi, Waamori, Wagirgashi, 17 oWahivi, Waariki, Wasini, 18 pWaarvadi, Wasemari na Wahamathi.
Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika, 19 qna mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.
20Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
Wazao Wa Shemu
21 rShemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.22 sWana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
23 tWana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
24 uArfaksadi alikuwa baba wa Shela,
naye Shela akamzaa Eberi.
25Eberi akapata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
26Yoktani alikuwa baba wa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 27 vHadoramu, Uzali, Dikla, 28 wObali, Abimaeli, Sheba, 29 xOfiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
30Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.
31Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
32Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.
Copyright information for
SwhNEN