Genesis 13:2-6
2 aWakati huo Abramu alikuwa tajiri sana wa mifugo, fedha na dhahabu.3 bKutoka Negebu, akapita mahali hadi mahali, hadi akafika Betheli, mahali hapo ambapo mwanzoni alipiga hema lake kati ya Betheli na Ai 4 chapo ambapo alikuwa amejenga madhabahu ya kwanza. Huko Abramu akaliitia jina la Bwana.
5 dBasi Loti, ambaye alikuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na makundi ya mbuzi, kondoo, ngʼombe na mahema. 6 eLakini nchi haikuwatosha kukaa pamoja kwa ajili ya wingi wa mali zao.
Copyright information for
SwhNEN