Genesis 22:11-15
11 aLakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!”Akajibu, “Mimi hapa.”
12 bAkamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”
13 cAbrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14 dAbrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire. ▼
▼Yehova-Yire maana yake Bwana atatupa.
Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.” 15 fBasi malaika wa Bwana akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili,
Copyright information for
SwhNEN