Jeremiah 2:23-35
23 a“Wawezaje kusema, ‘Mimi si najisi,sijawafuata Mabaali’?
Kumbuka jinsi ulivyotenda kule bondeni;
fikiri uliyoyafanya.
Wewe ni ngamia jike mwenye mbio
ukikimbia hapa na pale,
24 bpunda-mwitu aliyezoea jangwa,
anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa:
katika wakati wake wa kuhitaji mbegu
ni nani awezaye kumzuia?
Madume yoyote yanayomfuatilia
hayana haja ya kujichosha;
wakati wa kupandwa kwake watampata tu.
25 cUsikimbie hadi miguu yako iwe haina viatu,
na koo lako liwe limekauka.
Lakini ulisema, ‘Haina maana!
Ninaipenda miungu ya kigeni,
nami lazima niifuatie.’
26“Kama vile mwizi aaibikavyo wakati amekamatwa,
hivyo ndivyo nyumba ya Israeli inavyoaibishwa:
wao wenyewe, wafalme wao na maafisa wao,
makuhani wao na manabii wao.
27 dWanaiambia miti, ‘Wewe ndiwe baba yangu,’
nalo jiwe, ‘Wewe ndiwe uliyenizaa.’
Wamenipa visogo vyao
wala hawakunigeuzia nyuso zao;
lakini wakiwa katika taabu, wanasema,
‘Njoo utuokoe!’
28 eIko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea?
Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa
wakati mko katika taabu!
Kwa maana mna miungu mingi
kama mlivyo na miji, ee Yuda.
29 f“Kwa nini mnaleta mashtaka dhidi yangu?
Ninyi nyote mmeniasi,”
asema Bwana.
30 g“Nimeadhibu watu wako bure tu,
hawakujirekebisha.
Upanga wako umewala manabii wako
kama simba mwenye njaa.
31 h“Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la Bwana:
“Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli
au nchi ya giza kuu?
Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura,
hatutarudi kwako tena’?
32Je, mwanamwali husahau vito vyake,
au bibi arusi mapambo yake ya arusi?
Lakini watu wangu wamenisahau mimi,
tena kwa siku zisizo na hesabu.
33Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi!
Hata wale wanawake wabaya kuliko wote
wanaweza kujifunza kutokana na njia zako.
34 iKatika nguo zako watu huona
damu ya uhai ya maskini wasio na hatia,
ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba.
Lakini katika haya yote
35 junasema, ‘Sina hatia;
Mungu hajanikasirikia.’
Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema,
‘Mimi sijatenda dhambi.’
Copyright information for
SwhNEN