Jeremiah 25:15-38
Kikombe Cha Ghadhabu Ya Mungu
15 aHili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, aliloniambia: “Chukua kutoka mkononi mwangu kikombe hiki kilichojaa divai ya ghadhabu yangu, na kuyanywesha mataifa yote ambayo ninakutuma kwao. 16 bWatakapoinywa, watapepesuka na kukasirika sana kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka katikati yao.”17 cHivyo nikakichukua kikombe kutoka mkononi mwa Bwana, na kuyafanya mataifa yote aliyonituma kwao kukinywa: 18 dYaani Yerusalemu na miji ya Yuda, wafalme wake na maafisa wake, kuwafanya magofu na kuwa kitu cha kuchukiza, cha dhihaka na laana, kama walivyo leo; 19 epia Farao mfalme wa Misri, watumishi wake, maafisa wake na watu wake wote, 20 fpia wageni wote walioko huko; wafalme wote wa nchi ya Usi; wafalme wote wa Wafilisti (wale wa Ashkeloni, Gaza, Ekroni na watu walioachwa huko Ashdodi); 21 gEdomu, Moabu na Amoni; 22 hwafalme wote wa Tiro na Sidoni; wafalme wa nchi za pwani ngʼambo ya bahari; 23 iDedani, Tema, Buzi na wote walio maeneo ya mbali; 24 jwafalme wote wa Arabuni na wafalme wote wa watu wageni wanaoishi katika jangwa; 25 kwafalme wote wa Zimri, Elamu na Umedi; 26 lna wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali, mmoja baada ya mwingine; yaani falme zote juu ya uso wa dunia. Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshaki ▼
▼Sheshaki ni Babeli kwa fumbo.
atakunywa pia. 27 n“Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Kunyweni, mlewe na mtapike; angukeni, wala msiinuke tena kwa sababu ya upanga nitakaotuma miongoni mwenu.’ 28Lakini kama wakikataa kupokea kikombe kutoka mikononi mwako na kunywa, waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Ni lazima mnywe! 29 oTazama, nimeanza kuleta maafa juu ya mji ulio na Jina langu, na je, kweli ninyi mtaepuka kuadhibiwa? Hamwezi kuepuka kuadhibiwa, kwa maana nitaleta vita juu ya wote waishio duniani, asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.’
30 p“Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie:
“ ‘Bwana atanguruma kutoka juu;
atatoa sauti ya ngurumo
kutoka makao yake matakatifu
na kunguruma kwa nguvu sana
dhidi ya nchi yake.
Atapiga kelele kama wao wakanyagao zabibu,
atapiga kelele dhidi ya wote waishio duniani.
31 qGhasia zitasikika hadi miisho ya dunia,
kwa maana Bwana ataleta mashtaka dhidi ya mataifa;
ataleta hukumu juu ya wanadamu wote
na kuwaua waovu wote,’ ”
asema Bwana.
32 rHili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:
“Tazama! Maafa yanaenea
kutoka taifa moja hadi jingine;
tufani kubwa inainuka
kutoka miisho ya dunia.”
33 sWakati huo, hao waliouawa na Bwana watatapakaa kila mahali, kuanzia mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine. Hawataombolezewa wala kukusanywa au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyoenea juu ya ardhi.
34 tLieni na kuomboleza, enyi wachungaji,
mgaagae mavumbini,
ninyi viongozi wa kundi.
Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia;
mtaanguka na kuvunjavunjwa
kama vyombo vizuri vya udongo.
35 uWachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia,
viongozi wa kundi hawatapata mahali pa kutorokea.
36 vSikia kilio cha wachungaji, maombolezo ya viongozi wa kundi,
kwa maana Bwana anayaharibu malisho yao.
37Makao yao ya amani yataharibiwa
kwa sababu ya hasira kali ya Bwana.
38 wKama simba ataacha pango lake,
nchi yao itakuwa ukiwa
kwa sababu ya upanga wa mdhalimu,
na kwa sababu ya hasira kali ya Bwana Mungu.
Copyright information for
SwhNEN