‏ Job 18:5-21


5 a“Taa ya mwovu imezimwa,
nao mwali wa moto wake umezimika.
6 bMwanga hemani mwake umekuwa giza;
taa iliyo karibu naye imezimika.
7 cNguvu za hatua zake zimedhoofishwa;
shauri lake baya litamwangusha.
8 dMiguu yake imemsukumia kwenye wavu,
naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu.
9 eTanzi litamkamata kwenye kisigino;
mtego utamshikilia kwa nguvu.
10 fKitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake;
mtego uko kwenye njia yake.
11 gVitisho vimemtia hofu kila upande,
na adui zake humwandama kila hatua.
12 hJanga linamwonea shauku;
maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.
13 iNayo yatakula sehemu ya ngozi yake;
mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.
14 jAtangʼolewa kutoka usalama wa hema lake,
na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.
15 kMoto utakaa katika hema lake;
moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.
16 lMizizi yake chini itakauka
na matawi yake juu yatanyauka.
17 mKumbukumbu lake litatoweka katika dunia,
wala hatakuwa na jina katika nchi.
18 nAmeondolewa nuruni na kusukumiwa gizani,
naye amefukuzwa mbali atoke duniani.
19 oHana mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake,
wala aliyenusurika mahali alipoishi.
20 pWatu wa magharibi watashangaa yaliyompata;
watu wa mashariki watapatwa na hofu.
21 qHakika ndivyo yalivyo makao ya mtu mwovu;
ndivyo palivyo mahali pake mtu asiyemjua Mungu.”
Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.