Joel 1:10-18
10 aMashamba yameharibiwa,ardhi imekauka;
nafaka imeharibiwa,
mvinyo mpya umekauka,
mafuta yamekoma.
11 bKateni tamaa, enyi wakulima,
lieni, enyi mlimao mizabibu;
huzunikeni kwa ajili ya ngano na shayiri,
kwa sababu mavuno ya shambani yameharibiwa.
12 cMzabibu umekauka
na mtini umenyauka;
mkomamanga, mtende na mtofaa,
miti yote shambani, imekauka.
Hakika furaha yote ya mwanadamu
imeondoka.
Wito Wa Toba
13 dVaeni nguo ya gunia, enyi makuhani, muomboleze;pigeni yowe, enyi mnaohudumu madhabahuni.
Njooni, vaeni nguo ya gunia usiku kucha,
enyi mnaohudumu mbele za Mungu wangu;
kwa kuwa sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji
zimezuiliwa kufika katika nyumba ya Mungu wenu.
14 eTangazeni saumu takatifu;
liiteni kusanyiko takatifu.
Iteni wazee
na wote waishio katika nchi
waende katika nyumba ya Bwana Mungu wenu,
wakamlilie Bwana.
15 fOle kwa siku hiyo!
Kwa kuwa siku ya Bwana iko karibu;
itakuja kama uharibifu
kutoka kwa Mwenyezi. ▼
▼Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.
16Je, chakula hakikukatiliwa mbali
mbele ya macho yetu:
furaha na shangwe
kutoka nyumba ya Mungu wetu?
17Mbegu zinakauka
chini ya mabonge ya udongo.
Ghala zimeachwa katika uharibifu,
ghala za nafaka zimebomolewa,
kwa maana hakuna nafaka.
18Jinsi gani ngʼombe wanavyolia!
Makundi ya mifugo yanahangaika
kwa sababu hawana malisho;
hata makundi ya kondoo yanateseka.
Copyright information for
SwhNEN