‏ John 12:1-8

Maria Ampaka Yesu Mafuta Huko Bethania

(Mathayo 26:6-13; Marko 14:3-9)

1 aSiku sita kabla ya Pasaka, Yesu alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Yesu alikuwa anaishi. 2 bWakaandaa karamu kwa heshima ya Yesu. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Yesu. 3 cKisha Maria akachukua chupa ya painti moja
Painti moja ni kama nusu lita.
yenye manukato ya nardo
Nardo ni aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri.
safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Yesu na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.

4 fNdipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Yesu, akasema, 5“Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300
Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300.
na fedha hizo wakapewa maskini?”
6 hYuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.

7 iYesu akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu. 8 jMaskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.”

Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.