Matthew 24:3-14
Ishara Za Nyakati Za Mwisho
(Marko 13:3-23; Luka 21:7-24)
3 aYesu alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?”4 bYesu akawajibu, “Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye. 5 cKwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo,’ ▼
▼Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
nao watawadanganya wengi. 6 eMtasikia habari za vita na matetesi ya vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado. 7 fTaifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. 8Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu. 9 g “Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu. 10 hWakati huo, wengi wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchukiana. 11 iWatatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi. 12Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa, 13 jlakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa. 14 kInjili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja.
Copyright information for
SwhNEN