‏ Matthew 3:1-5

Yohana Mbatizaji Atayarisha Njia

(Marko 1:1-8; Luka 3:1-18; Yohana 1:19-28)

1 aSiku hizo Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Uyahudi, akisema, 2 b“Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.” 3 cHuyu ndiye yule aliyenenwa habari zake na nabii Isaya aliposema:

“Sauti ya mtu aliaye huko nyikani,
‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.’ ”
4 dBasi Yohana alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia, akiwa na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 5 eWatu walikuwa wakimwendea kutoka Yerusalemu, Uyahudi yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani.
Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.