Numbers 28:3-11
3 aWaambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea Bwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku. 4 bAndaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni, 5 ckila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa ▼▼Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja.
ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini ▼▼Robo ya hini ni sawa na lita moja.
ya mafuta ya zeituni. 6 fHii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. 7 gSadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwa Bwana mahali patakatifu. 8 hAndaa yule mwana-kondoo wa pili jioni, pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kama ulivyofanya kwa ile sadaka nyingine ya asubuhi. Hii ni sadaka iliyotolewa kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. Sadaka Za Sabato
9 i“ ‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi za efa ▼▼Sehemu mbili za kumi za efa ni sawa na kilo 2.
za unga laini uliochanganywa na mafuta. 10 kHii ni sadaka ya kuteketezwa itakayotolewa kwa ajili ya kila Sabato, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya kinywaji. Sadaka Za Kila Mwezi
11 l“ ‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamletea Bwana sadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari.
Copyright information for
SwhNEN