Numbers 34:2-12
2 a“Waamuru Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia nchi ya Kanaani, nchi ambayo itagawanywa kwenu kama urithi itakuwa na mipaka ifuatayo:3 b“ ‘Upande wenu wa kusini utajumuisha sehemu ya Jangwa la Sini kufuata mpaka wa Edomu. Upande wa mashariki mpaka wenu wa kusini utaanzia mwisho wa Bahari ya Chumvi, ▼
▼Yaani Bahari Mfu.
4 dkatiza kusini mwa Pito la Akrabimu, endelea mpaka Sini na kwenda kusini ya Kadesh-Barnea. Kisha mpaka huo utaenda hadi Hasar-Adari hadi Azmoni, 5 emahali ambapo utapinda, na kuunganika na Kijito cha Misri na kumalizikia kwenye Bahari ya Kati. ▼▼Yaani Mediterania.
6 g“ ‘Mpaka wenu wa magharibi utakuwa Bahari ya Kati. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa magharibi.
7 h“ ‘Kwa mpaka wenu wa kaskazini, wekeni alama kuanzia Bahari ya Kati hadi mlima Hori, 8 ina kutoka mlima Hori hadi Pito la Hamathi. Kisha mpaka utaenda hadi Sedadi, 9 jkuendelea hadi Zifroni, na kuishia Hasar-Enani. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa kaskazini.
10 k“ ‘Kwa mpaka wenu wa mashariki, wekeni alama kuanzia Hasar-Enani hadi Shefamu. 11 lMpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye miteremko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi. ▼
▼Yaani Bahari ya Galilaya.
12Kisha mpaka utashuka kuelekea Mto Yordani na kuishia katika Bahari ya Chumvi.“ ‘Hii itakuwa nchi yenu, ikiwa na mipaka yake kila upande.’ ”
Copyright information for
SwhNEN