Psalms 35:1-8
Kuomba Msaada: Kuokolewa Kutokana Na Maadui
Zaburi ya Daudi.
1 aEe Bwana, pingana na wale wanaopingana nami,upigane na hao wanaopigana nami.
2 bChukua ngao na kigao.
Inuka unisaidie.
3Inua mkuki wako na fumo ▼
▼Fumo ni sawa na sagai, maana yake ni mkuki mfupi.
lakodhidi ya hao wanaonifuatia.
Iambie nafsi yangu,
“Mimi ni wokovu wako.”
4 dWafedheheshwe na waaibishwe
wale wanaotafuta uhai wangu.
Wanaofanya shauri kuniangamiza
warudishwe nyuma kwa hofu.
5 eWawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,
malaika wa Bwana akiwafukuza.
6Njia yao na iwe giza na ya utelezi,
malaika wa Bwana akiwafuatilia.
7 fKwa vile walinifichia wavu wao bila sababu,
na bila sababu wamenichimbia shimo,
8 gmaafa na yawapate ghafula:
wavu walionifichia na uwatege wenyewe,
na waanguke katika shimo hilo,
kwa maangamizo yao.
Copyright information for
SwhNEN