Psalms 72:6-11
6 aAtakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa,kama manyunyu yanyeshayo ardhi.
7 bKatika siku zake wenye haki watastawi;
mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.
8 cAtatawala kutoka bahari hadi bahari
na kutoka Mto ▼
▼Yaani Mto Frati.
mpaka miisho ya dunia.9Makabila ya jangwani watamsujudia,
na adui zake wataramba mavumbi.
10 eWafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali
watamletea kodi;
wafalme wa Sheba na Seba
watampa zawadi.
11 fWafalme wote watamsujudia
na mataifa yote yatamtumikia.
Copyright information for
SwhNEN