‏ Revelation of John 18:16-19

16 a“ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa,
uliyekuwa umevikwa mavazi ya kitani safi,
ya rangi ya zambarau na nyekundu,
ukimetameta kwa dhahabu,
vito vya thamani na lulu!
17 bKatika muda wa saa moja utajiri wote mkubwa
kama huu umeangamia!’
“Kila nahodha, na wote wasafirio kwa meli, na wote wapatao kipato chao kutokana na bahari, watasimama mbali.
18 cWatakapouona moshi wa kuungua kwake watalia wakisema, ‘Je, kulipata kuwako mji mkubwa kama huu?’ 19 dNao watajirushia mavumbi vichwani mwao, huku wakilia na kuomboleza, wakisema:

“ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa,
mji ambao wote wenye meli baharini
walitajirika kupitia kwa mali zake!
Katika saa moja tu ameangamizwa!
Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.